Picha zote na Raymond Mihayo-Kahama
Mvua kubwa iliyonyesha jana jioni mjini Kahama Mkoani Shinyanga imesababisha dhahama kubwa baada ya kuingia ndani ya nyumba za watu za biashara na makazi ya wanachi wa mji wa Kahama kama vile katika benki, Hoteli na nyumba za kulala wageni lakini pia ikawa taabu kweli kweli kwa vyombo vya usafiri kama magari na pikipiki kupita.
Mvua hiyo iliyonyesha kwa muda wa takribani saa moja imebomoa pia ukumbi mmoja wa Hotel ya Mamba huku watu kibao watu waliokuwa ndani ya ukumbi huo wakinusurika.
Lakini pia kwa taarifa ambazo bado hazijathibitishwa kuna matukio ya watu kujeruhiwa na radi ambazo zilikuwa zikiambatana na mvua hiyo.
Social Plugin