Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangala |
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga
limesema katika kuhakikisha wanachi wake wanasherehekea sikukuu ya chrismas na
mwaka mpya limeandaa vikosi kazi kwa ajili ya kukabiliana na wahalifu wanaotumia
msimu wa sikukuu kufanya uhalifu wa aina mbalimbali ikiwemo kuvamia na kupora mali za
wananchi
Akizungumza na waandishi wa habari
mapema leo Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangala
amesema vikosi kazi hivyo vitasambaa kila wilaya vikifanya doria na msako mkali
ili kuhakikisha kuwa wananchi wanasherehekea sikukuu kwa amani na utulivu
“Mwaka huu tumeamua kuja na staili yetu hapa
Shinyanga kwani katika msimu wa sikukuu wahalifu wamekuwa wakipanga mbinu za kuvamia majumbani
kwa wananchi kwa lengo la kuwapora mali ,na
na vikosi kazi hivi vitafanya kazi
hadi mwezi wa kwanza”,aliongeza Kamanda.
Kamanda Mangala ametumia fursa hiyo
kuwaonya watu wanaomiliki silaha kihali
na kutumia kinyume na taratibu mfano kujeruhi na kutishia wenzao jeshi la polisi halitasita kunyang’anya silaha kwa
kufuata taratibu na sheria.
Aidha amewataka wananchi pindi wanapokwenda
kwenye sehemu za starehe wasiache nyumba zao pekee bila ya kuwa na mwangalizi
ili kutowapa mianya wahalifu kupora mali zao na kutoa taarifa pindi
wanapohisi kuna uvunjifu wa amani unataka kufanyika.
Social Plugin