Mwili wa moja ya majambazi yaliuawa mkoani Singida ukiwa katika hospitali ya mkoa huo |
Mwili wa jambazi jingine lililouawa Singida
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela,akionyesha
bunduki ya kijeshi aina ya SMG no.34555 iliyokuwa ikitumiwa na watu
wawili wanaodhaniwa kuwa majamabazi katika kijiji cha Manga manispaa ya Singida
Jeshi la Polisi mkoani Singida limewauwa watu wawili wanaodhaniwa
kuwa ni majambazi wakati wa kurushiana rasasi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, SACP, Geofrey Kamwela
amesema tukio hilo limetokea Desemba 9 mwaka huu saa 12:00 jioni, huko katika
kijiji cha Manga nje kidogo ya mji wa Singida.
Amesema watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na bunduki
moja ya kijeshi aina ya SMG, walifika kijijini hapo kwa lengo la kufanya
uhalifu.
Akielezea zaidi kuhusu tukio hilo, amesema taarifa za siri kutoka kwa
raia wema zililifikia jeshi la polisi na ndipo askari polisi walipofika kwenye
eneo la tukio.
“Baada ya polisi kufika kijijini hapo watu hao walishtuka kuwa
wanafuatiliwa na askari polisi na hivyo kuanza kukimbia kuelekea kijiji cha
Uhamaka kwa kutumia pikipiki yenye namba za usajili T. 634 BTW aina ya Sanlag
yenye rangi nyeusi”,amesema Kamwela.
“Hali ilipokuwa ngumu zaidi, walianza kuwarushia polisi risasi, hivyo
polisi nao ikwabidi kujibu mapigo na katika majibizano hayo ya
risasi, majambazi mawili yaliweza kujeruhiwa huku mmoja akifanikiwa kutoroka",aliongeza.
Amesema majambazi hayo yaliyojeruhiwa yalifariki dunia njiani wakati
yanakimbizwa katika hospitali ya mkoa kwa matibabu.
Amesema katika eneo la tukio, ilipatikana bunduki moja aina ya SMG
yenye namba 34555 ikiwa na risasi saba kwenye magazine. Pia pikipiki
iliyokuwa inatumiwa na majambazi hayo na ilipatikana.
Kamwela ametoa wito kwa wananchi kuendelea na moyo huo huo wa
kuwafichua watu wanaowatilia shaka ili waweze kudhibitiwa mapema kabla ya
kufanya uhalifu.
Chanzo-Chami wa Matukio blog
Social Plugin