Familia ya mzee Luhemeleja mkoani Geita iliyovamiwa kisha kuporwa pesa za rambi rambi kisha watuhumiwa kuchomwa moto wiki iliyopita |
Mzee John Luhemeleja akiwa katika hospitali ya wilaya ya Geita akipatiwa matibabu |
Familia ya mzee John Luhemeja [68]iliyovamiwa na kunyang’anywa rambirambi kiasi cha shilingi elfu 56 iliteswa kinyama baada ya kufungwa kamba yeye na mke wake Roza Kisinza (43)na kulazwa kifudifudi huku mwanamke akiwa mtupu na mme akiwa amevaa bukta pekee walimochukua pesa zile.
Akisimulia
mkasa huo Mzee Luhemeja akiwa katika
Hospital ya wilaya Geita
Wodi No [8] alikolazwa akiuguza majeraha yake sehemu za kichwani na mdomoni
amesema kuwa”akiwa amelala nyumbani kwake muda saa sita alisikia sauti ya mbwa
anabweka nje ya nyumba yake akatoka nje akiwa na mkuki.
Alipotoka nje
akakutana na kijana wake Kamuri John(6) anatoka kujisaidia akiwa amepigwa kofi
na kuambiwa arudi ndani huku mzee akimrikwa tochi machoni na wezi hao na kushtukia anampigwa ubapa wa panga
na kumuangusha hapo hapo .
Amesema wakiwa
wanamsulubu walimwamuru atoe pesa alizonazo na yeye akipiga kelele ndipo mke
wake aliposikia kelele hizo akatoka nje na kumkuta mme wake anapigwa akiwa
ameangushwa chini………..
Ameongeza kuwa
baada kutoka nje wezi hao waliwaamuru kurudi ndani wote huku wakiwa wamefungwa
kamba kwenye mikono kwa nyuma na wakaambiwa kulala kifudifudi baada ya kipigo
kuzidi mzee Luhemeja aliwaambia wafungue zipu kwenye kaptula ndipo wakakuta
kiasi cha shilingi elfu 60 za rambirambi na kuzichukua.
Hawakuishia
hapo lakini pia watu hao walimwamuru mke wa Luhemeja atoe pesa alizonazo naye
akawanbia hana lini kipigo kilipozidi aliwaambia wachukue kwenye begi kuna
shlingi elfu 5 aliyopewa jioni hio na waliokuja kumhani huku akiwa uchi wa
mnyama na kamba zake….
Mzee Luhemeja
ameendelea kusema kuwa baada ya kumaliza waliingia kwenya chumba cha mabinti
walimokuwa wamelala na kuwataka watoe pesa ambapo walitoa kiasi cha shilingi
elfu 80 na simu moja ya mkononi na majina yao
ni Semeni John miaka[23]
Siwema John [16] na Kurwa John [14] wote walikuwa wamelala kwenye chumba hicho.
Baada ya watoto
hao kutoa pesa na simu wakachukuliwa na kupelekwa kweye chumba cha wazazi wao
waliokuwa wamelazwa kifudifudi nao wakaamuliwa kulala kifudifudi…..
Tukio hilo lilidumu kwa
takribani saa moja majambazi hao waliamua kutoka na kuwafungia mlango kwa nje huku wakiamuriwa wasipige kelele
na wakipiga kelele wanawamaliza papo hapo.
Mzee huyo
amesema baada ya muda mfupi mzee huyo aliomba afunguliwe kamba huku mke wake
akisema asipige kelele watarudi kuwamaliza kwa vile mzee luhemeja alikuwa
amechoka alimwambia mke wake acha watumalize tu ndipo mke wake akalegeza kamba
zake na kujifungua na kisha kumfungulia mme wake……
Baada ya
kufunguliwa waliwaita watoto wao waliokuwa nyumba nyingine na kuwafungulia mlango na
kumkuta Baba yao
yuko hoi akiwa amekatwakatwa mapanga ndipo wakaita majirani wa karibu
wakakusanyika na kupiga yowe huku mzee luhemeja akipelekwa Hospitali ambako amelazwa
mpaka sasa akiendelea na matibabu……..
Baada ya yowe
kuwa kubwa wananchi walikusanyika na kuanza kuwasaka waliohusika na kitendo
hicho na walipowapata walianza kutajana mmoja baada ya mwingine na kufikia wananchi
kuwapiga na kuwachoma moto huku wakisema wamechoshwa na vitendo
hivyo”…………alisema mzee luhemeja.
Naye katibu wa Geita Legal Aid
Center Bw,Elineema Charles anayeshughulika na utetezi wa haki za binadamu
wilayani Geita amesema kuwa ni kitendo ambacho hakivumiliki cha watu
kujichukulia sheria mikononi kwa kuua raia kama walivyofanya wakazi wa Geita
kwa kuua watu hao watano kwani huo ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na
kwamba mahakama imenyang’anywa mamlaka yake ya kutoa haki.
Kwa upande wa mkuu wa mkoa wa Geita
aliyefika kwenye eneo la tukio Bw Said Magalula amekeme vikali kitendo cha
wananchi kujichukuli sheria mkononi na kulitaka jeshi la polisi kuwakamata wote
walihusika na mauaji hayo ya kikatili ili sheria ichukue mkondo wake.
Na Valence
Robert- Geita
Social Plugin