Hatimaye utabiri uliotabiriwa na mtume TB Joshua wa Nigeria mwezi Octoba mwaka huu juu ya kiongozi mkuu wa moja ya nchi za Afrika mashariki kutekwa huku akikataa kutaja jina la nchi hiyo ila akisema iko karibu na Kenya zaidi ya kuwataka watu kufunga na kuomba juu ya nchi hiyo. Hatimaye utabiri huo umetimia kwa kiongozi wa Sudan ya kusini ambako kuna mapigano kwasasa.
Kiongozi huyo amezungumzia juu ya utabiri wake huo katika ibada ya jumapili iliyopita kanisani kwake SCOAN nchini Nigeria ambapo Rais wa Sudan ya kusini alituma ujumbe wa watu wawili na barua ya shukrani kwa nabii huyo kwa utabiri wake juu ya taifa hilo ambapo akamuomba nabii huyo kuliombea taifa lake kuwepo mapatano na kuahidi kufika SCOAN mambo yatakapotulia. Tazama video hapo juu kwa maelezo zaidi.
Social Plugin