WAFANYABIASHARA WA GEITA WATAKIWA KUTOKIMBIA NDANI,KILA KITU KINAWEZEKANA HUMO HUMO MKOANI GEITA

Wafanya biashara katika mkoa wa geita wametakiwa kuwekeza kwenye mkoa wao kuliko kuwekeza mikoa mingine ili maendeleo ya mkoa huo yaweze kukua kwa haraka na kuacha malumbano na majungu yasiyo kuwa na msingi 

kauli hiyo imetolewa jana na Kaimu mkuu wa mkoa Geita ambaye ni mkuu wa wilaya Geita Bw. Omary Manzie Mangochie kwenye hafra fupi ya uzinduzi wa ukumbi wa mikutano iliyo fanyika katika ukumbi huo ulioko mjini Geita 

Bw. Mangochie ambaye alikuwa ni mgeni rasimi kwenye uzinduzi huo amewataka wafanya biashara wakubwa na wadogo wadogo wa mkoa huo kuwekeza kuliko kuwekeza mkikoa mingine ili mkoa ukue wa kasi na uwe na vivutio vya aina mbalimbali pamoja na hayo aliwaomba wananchi wengine kuiga mfano wa Endrwe shilima kwa fungua ukumbi wa mikutano ya aina mbalimbali 

"Mimi kama mkuu wa wilaya nitahakikisha natoa ushirikiano mzuri kwa wafanya biashara wa mkoa huu kuwashauri wasiwekeze mbali na badala yake wawekeze kwenye mkoa wetu alisema Bw.Mangochie"

Naye mkurugenzi wa ukumbi huo Bi Aldegunda Lakataya amesema pamoja na kutaka kujenga vivutio mbalimbali katika mkoa wa Geita lakini wanakumbana na changamoto mbalimbali kama kukosa viwanja na kodi ikiwa kubwa na hivyo kuiomba serikari kuweza kushirikiana na wafanya bishara ili kuangalia jinsi ya kupunguza changamoto hizo

" Mfano hapa Geita kuna kisiwa cha Rumbondo National Park ambacho serikari ikishirikiana na wafanya bishara kinaweza kikawaingizia pato kubwa watu wa Geita pamoja na watanzania kwa ujumla alisema Bi Aldegunda Lakataya Mkurugenzi wa ukumbi huo utakaohudumia zaidi ya watu 1000 na ukiwa ni wa kwanza kujengwa katika mkoa wa Geita.

 Na Valence Robert

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post