Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAKANDARASI WAICHAFUA MANISPAA YA SHINYANGA,TENDA ZAKE NI ZA UBABAISHAJI,NAIBU MEYA AGEUKA MBOGO

Mmoja wa wakandarasi  waliohudhuria kikao cha halmshauri ya manispaa ya Shinyanga na wakandarasi wa manispaa bwana  Erasto Kwilasa ambaye pia ni mtendaji na mweka hazina wa chama cha wakandarasi mkoa wa Shinyanga akizungumza katika kikao hicho awali kabla hakijavunjika.Pamoja na mambo mengine alisema manispaa ya Shinyanga imegubikwa na wimbi la ubabaishaji katika kugawa tenda hali inayowapa mashaka wakandarasi hao na kujikuta wakati mwingine kuogopa kufanya kazi na manispaa hiyo.Lakini pia aliongeza kuwa kikao hicho hakikuwa na msaada kwao kama wakandarasi kutokana na walengwa wakuu kama vile mkurugenzi wa manispaa hiyo Festo Kang'ombe kutokuwepo katika kikao hicho.
Hata hivyo mambo yalibadilika ghafla baada ya naibu mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila(aliyeko kulia) kuingia katika kikao hicho na kuhoji kwanini kikao kinaendelea wakati kimsingi yeye ndiye aliyeitisha kikao hicho kwani ofisi ya mkurugenzi imeingilia kikao chake na kumruhusu kaimu mkurugenzi Boniface Maheri(Kushoto) aendeshe  kikao wakati mwenye kikao hajapewa taarifa kuwa kikao kiko tayari kuanza.Naibu meya huyo alisema kufuatia malalamiko aliyopokea kutoka kwa wakandarasi kuhusu manispaa yeye binafsi kwa kutumia ubunifu wake aliomba kukutana na wakandarasi ili kuzungumza nao ili kujua nini kinawakwamisha na pengine kujikuta wakifanya kazi chini ya kiwango kinachotakiwa.Lakini akasema kufuatia ofisi ya mkurugenzi kumzunguka katika kikao hicho na kukifanya chake inampa mashaka .
Baadhi wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia alichokuwa anazungumza naibu meya David Nkulila ambapo Naibu meya huyo alisema kutokana na ufuatiliaji wake na kupenda haki na ukweli amekuwa akionekana kikwazo kwa baadhi ya watendaji kazi katika manispaa ya Shinyanga na ndiyo maana hata kikao hicho wamemwingilia japokuwa alikuwa katika chumba cha pili kutoka ukumbini)pengine kukwepesha ukweli kuhusu wakandarasi ambao wamekuwa wakiilalamikia manispaa hiyo hususuni katika suala la ugawaji wa tenda hivyo kuhisi pengine kuna kitu kinaendelea kwa watendaji hao wa manispaa ya Shinyanga

Baadhi wa waandishi wa habari waliokuwa ndani ya ukumbi wa manispaa ya Shinyanga wakichukua mawilia matatu yaliyokuwa yanajiri katika ukumbi huo ikiwa ni pamoja na wakandarasi hao kuomba kikao kiahirishwe kutokana na kwamba waliohudhuria walikuwa wachache na hali ya kutwepo kwa sintofahamu kati ya ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga pamoja na ofisi ya mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga.Japokuwa kwa mujibu wa taarifa ya kaimu mkurugenzi Maheri alisema hali ya mstahiki meya ambaye ndiyo mwenye kikao kutoitwa kikaoni ni tatizo tu la mawasiliano.

Wajumbe wa kikao hicho wakisikiliza kilichokuwa kinaendelea 

Naibu mstahiki meya David Nkulila  akizungumza mara baada ya wakandarasi kuomba kuahirishwa kwa kikao hicho.Nkulila amesema ataitisha mkutano wake na wakandarasi ndani ya mwezi Januari 2014 ili kuwasikiliza na kuzungumza nao kujua changamoto mbali mbali zinazowakabili ili kuhakikisha kuwa wanondoa kero,kuleta usawa na ufanisi katika utendaji kazi pamoja na kwamba watendaji wa manispaa hiyo wanamkwepa kwepa kutokana na hali yake ya ufuatiliaji na kusimamia ukweli

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com