Rais Kikwete |
Waziri Chiza
|
Baada ya Rais Kikwete
kutengua uteuzi wake kwa mawaziri wa mambo ya ndani ya nchi, maliasili na
utalii, ulinzi na mifugo na uvuvi ,wakulima wa zao la pamba mikoa ya Shinyanga
na wamemwomba Mheshimiwa rais kumwajibisha pia kwa waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika,
Mhandishi Christopher Chiza.
Wakulimahao wamesema Chiza hana budi kuwajibishwa
kutokana na kitendo chake cha kuruhusu matumizi ya mbegu za pamba
zinazosambazwa na kampuni ya Quton,zisozokuwa na manyoya ambazo zimegoma kuota
katika maeneo mengi katika mikoa ya Shinyanga, Tabora, Geita na Simiyu na
kusababisha hasara kwa wakulima hao na hawalipwi fidia kutokana na hasara hiyo.
Naye
katibu wa Chama cha wakulima wa zao la
pamba wilayani Kahama (TACOGA), Paulo Ntelya amesema waziri Chiza ni mmoja wa
mawaziri waliolalamikiwa na wakulima wa zao la korosho wakati wa ziara ya
katibu mkuu wa CCM Taifa, Abdurahman Kinana alipokuwa katika ziara ya mikoa ya
kusini na kwamba hata CCM wenyewe walipendekeza waziri huyo awajibishwe.
Social Plugin