Watu watatu akiwemo mtoto wa miaka saba wamejeruhiwa kwa
kupigwa na radi katika sehemu mbalimabali za miili yao katika kijiji cha Nyakafuru kata ya
Nayakafuru tarafa ya Masumbwe wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita Leonard Paul amesema tukio hili limetokea Desemba 13 mwaka
huu majira ya saa nane mchana katika kijiji hicho ambapo watu hao watatu
walipigwa radi.
Amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Paulo Lwelwe(39) bi Mwamba Paulo(18) na mtoto
aitwaye Kiumbe Paulo(7) ambao wote walipigwa na radi wakati wakiwa nyumbani
kwao wakati mvua ikinyesha katika kijiji
hicho.
Kamanda Paulo amesema majeruhi wote wamelazwa katika kituo
cha afya cha Masumbwe kwa ajili ya matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.
Na Valence
Robert -Geita
Social Plugin