Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ZAHANATI YA AKINA MAMA WAJAWAZITO YAGEUZWA MAKAZI YA POPO


Serikali imetakiwa kuingilia kati jengo lililojengwa kwenye zahanati ya kijiji cha Kerende Kata ya Kemambo Wilayani Tarime mkoani Mara kwa msaada wa Benk ya Maendeleo Afrika (African Development Bank)

Jengo hilo ambalo limejengwa kwa ajili ya huduma ya akina mama na watoto hadi sasa halijakabidhiwa na kusababisha popo kuendelea kuishi na kushamili ndani ya jengo kutokana na  jengo hilo kukaaa muda mrefu bila kutumika.

 Mwenyekiti wa Kijiji cha Kerende Mambaga Mohamed amesema Zahanati ya Kerende haina jengo la huduma ya wajawazito hivyo huduma huipata nje ya jengo la Zahanati kutokana na uhaba wa vyumba vya kutolea huduma ya afya.

Ameiomba  serikali kuwafuatilia wafadhili ili kukamilisha jingo hilo ambalo hivi sasa limegeuka makazi ya popo.

 Mganga Mkuu Hospitali ya Wilaya ya Tarime Charle Samson amesema  ofisi yake haifahamu gharama zilizotumika katika ujenzi kwa kuwa wafadhili hawakuishirikisha idara ya afya na kwamba jengo hilo limejengwa chini ya viwango vinavyotakiwa.

        Credit Mara yetu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com