Bi.
Kizee akiwa kwenye gari la polisi baada ya kuokolewa na polisi kutoka
kwa wananchi wenye asila kali mara tu ya kukutwa kwenye chumba.
Bi. Kizee anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70, ambaye
jina lake
halikuweza kufahamika kwa urahisi amenusurika kifo baada ya polisi kumnusuru kwa kudaiwa kukutwa akiwa uchi
chumbani kwa mtu
akifanya mambo yasiyoeleweka alfajiri ya leo Ijumaa Januari 31,2014
Mashuhuda wa mwanzo wanasema Bibi huyo amekutwa akitapatapa bila kujua
la kufanya huku mwili wake ukiwa Uchi na nguo zake zikiwa pembeni kitendo kinachopelekea kusadikiwa kwamba Bibi huyu ni mchawi wakati wengine wakisema wasubiri taarifa ya Polisi.
PICHA ZOTE NA BUKOBAWADAU BLOG
Polisi wakiondoka eneo la tukio wakiwa na Shuhuda mmoja aliyedai alikuwa miongoni mwa watu waliomkurupusha bibi huyo chumbani.
Wakielekea kituo cha cha polisi cha Bukoba Mjini leo asubuhi.
Bibi huyo akiwa kwenye ulinzi mkali baada ya kufikishwa kwenye kituo kikuu cha polisi mjini Bukoba
Social Plugin