Habari za hivi punde zilizoufikia
mtandao huu wa malunde1.blogspot.com zinasema kuwa Wanafunzi wanne Wa shule ya sekondari Mustapha Sabodo mjini Mtwara wamekufa na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa baada ya kugongwa na gari aina ya Benzwakiwa kwenye mchakamchaka asubuhi ya leo.
Tukio hjilo limetokea leo majira ya saa asubuhi wakati
wanafunzi hao wakikimbia mchaka mchaka.
Chanzo cha ajali hiyo kinatokana na gari dogo aina ya Benzi
kumgonga mwanafunzi mmoja aliyekuwa kwenye mchakamchaka na katika hali ya
taharuki ya mwenzao bila kuangalia nyuma ndipo lori jingine likawagonga wanafunzi wengine na
kusababisha mwanafunzi mmoja kufariki dunia papo hapo na wengine watatu
wakifariki hospitali wakati wakipatiwa matibabu huku majeruhi wakiwa 20.
Dreva wa Benzi amejisalimisha kituo cha polisi Mtwara lakini
Yule wa Lori amekimbia.
Social Plugin