Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

FUATILIA HAPA KILICHOJIRI LEO KATIKA BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA

Mwenyekiti wa baraza la madiwani wa manispaa ya Shinyanga,ambaye ni naibu mstahiki meya wa manispaa hiyo Bwana David Nkulila akizungumza katika baraza hilo lililofanyika leo katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga mjini Shinyanga ambapo alisema miongoni mwa changamoto zinazoikabili manispaa hiyo ni suala la baadhi ya watendaji wa manispaa hiyo kuihujumu manispaa kwa kushiriki katika kufungua kesi kuishtaki manispaa lengo likiwa ni kujipatia pesa katika njia zisizokuwa sahihi.
 Wa kwanza kulia ni mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Festo Kang'ombe.Aliyesimama ni katibu tawala wilaya ya Shinyanga Boniface Chambi akizungumza katika kikao hicho cha madiwani ambapo amekemea vikali tabia ya baadhi ya watendaji wa manispaa kutoa siri za ofisi na kuhujumu manispaa hiyo na kuongeza kuwa yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani zitafanyika.
Wajumbe wa kikao cha maadiwani wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika baraza hilo ndani ya ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga 
Aliyesimama na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Ndugu Anna rose Nyamubi akizungumza katika baraza hilo la madiwani ambapo pamoja na mambo mengine amesema suala kuwasaidia watoto wenye ulemavu wanaoishi katika kituo cha Buhangija jumuishi katika manispaa ya Shinyanga ni watu wote katika jamii na taifa kwa ujumla hivyo kuzikumbusha halmashauri mbalimbali zinazopeleka watoto wenye ulemavu wakiwemo walemavu wa ngozi kama vile halmashauri ya wilaya ya Bukombe ambayo imeleta watoto 39 hadi sasa kutoa msaada badala ya kuitelekezea manispaa ya Shinyanga jukumu la kuwalea watoto hao kwani wanahitaji msaada zaidi

Diwani wa kata ya Ngokolo kupitia tiketi ya CHADEMA Sebastian Peter akichangia mawili matatu kuhusu watoto wenye ulemavu katika kituo cha Buhangija ambapo amesema kama halmashauri zinapeleka watoto wake katika kituo hicho halafu hawatoi msaada kwa watoto hao baso waje wachukue watoto wao.Lakini pia amesema tatizo la kuendelea kuwepo kwa changamoto katika kituo hicho linatokana na mwalimu mkuu wa shule ya Buhangija walipo watoto hao kufanya mambo kwa siri ,wafadhili wanakuja yeye hatoi taarifa hata kwa idara husika hazipewi taarifa pia misaada inatolewa halafu wanapokea kimya kimya

Kikao kinaendelea waalikwa katika kikao hicho wakisikiliza kwa umakini kilichokuwa kinajiri

Mkurugenzi wa mamlaka ya maji katika manispaa ya Shinyanga Eng. Silvester Mahole akizungumzia suala la kituo cha Buhangija jumuishi walipo watoto wenye ulemavu kudaiwa mamilioni ya fedha ambapo alisema deni haliwezi kufutika na kuzishauri mamlaka zinazohusika kuangalia namna ya kubadili jina la akaunti badala ya kutumia jina la mwalimu mkuu wa shule ya msingi Buhangija na kwamba siku zilizopita waliamua kuwakatia huduma ya maji ili kujua nani hasa anahusika na suala la maji katika kituo hicho kutokana na jambo hilo kutolielewa vyema


Madiwani wakifuatilia kikao hicho

Kikao kinafungwa na mwenyekiti wake bwana David Nkulila ambaye ni naibu meya wa manispaa ya Shinyanga ambapo alisisitiza suala la uwajibikaji kwa kila mmoja ili kufikia mafanikio yanayohitajika

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com