Ikiwa ni siku chache tu baada ya Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele ambaye pia ni naibu waziri wa madini kufanya mkutano wa hadhara mjini Shinyanga na kusema kusema kuwa madiwani wa CHADEMA wamekuwa mzigo katika jimbo lake, Madiwani wa chama cha Demokrasia na Maendelao CHADEMA katika manispaa ya shinyanga wamekanusha tuhuma zilizotolewa dhidi yao na mbunge wa jimbo la shinyanga mjini Stephen Masele kuwa madiwani wa chama hicho ni mizigo katika jimbo lake kutokana na kushindwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo
Madiwani hao wa CHADEMA waliyasema hayo jana mjini Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara ambao waliuitisha kwa lengo la kujibu tuhuma ambazo amekuwa akitoa mbunge huyo mbele ya wananchi mfano katika mkutano wa mwezi uliopita katika viwanja vya mahakama ya mwanzo mjini Shinyanga Masele alisema kwamba madiwani wa CHADEMA katika jimbo la Shinyanga mjini wamekuwa mzigo kwa kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo kama vile ujenzi wa zahanati.
Madiwani hao wamesema wao sio mizigo kutokana na kwamba katika kata zao tayari wameshawaletea maendeleo wananchi lakini mbunge huyo kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM amekuwa akiwachafua kwenye mikutano yake ya hadhara badala ya kuangalia changamoto gani wanazokabiliana nazo madiwani hao.
Diwani wa kata ya Masekelo Zacharia Martin amesema mtu unapochaguliwa kuwa mbunge unatakiwa kuwasikiliza madiwani wote pamoja na kutatua changamoto zao kwani wao ndio wawakilishi wa wananchi na siyo kuwabagua kama anavyofanya Mbunge huyo wa Shinyanga mjini na kuwasema vibaya madiwani wa Chadema katika majukwaa kwamba hawafanyi kazi.
Martin alisema licha ya mbunge huyo kumpatia mifuko mia moja ya saruji kwa ajili ya kujenga zahanati katika kata yake lakini imeshindikana kutokana na eneo linalotakiwa kujengwa wananchi bado hawajalipwa fidia hivyo kumwia vigumu kutekeleza mradi huo.
Naye Diwani wa kata ya Ndala John Sungura aliyekuwa anatuhumiwa kula mifuko mia moja ya soko kuu Ndala amesema tangu achaguliwe kuwa Diwani hajawahi kumuona mbunge huyo akihudhuria hata siku moja kwenye kikao cha baraza la madiwani wa manispaa hiyo ndio maana hata miradi mingine ya maendelo anakuwa haijui pamoja na migogoro hiyo ya ardhi na kusemakuwa anatakiwa kuwa anahudhulia kwenye vikao hivyo ilikujua madiwani wake wanafanya nini
Social Plugin