Majanga!!!! JAMAA APANDA JUU YA MNARA WA SIMU ,AGOMA KUSHUKA MPAKA RAIS KIKWETE AJE ASIKILIZE KERO ZAKE...!!!
Wednesday, January 01, 2014
Mwanaume mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja amepanda juu ya mnara wa kampuni ya simu za
mkononi ya Vodacom uliopo Ubungo katika eneo la ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) jijini Dar es Salaam na kutaka kujirusha.
Katikakati jamaa akiwa juu ya mnara
Wananchi wakimwangalia jamaa akiwa juu ya mnara wa simu
Wakazi wa Dar es salaam waliofika eneo la tukio
Jamaa akizungumza na wanahabari katika eneo la tukio baada ya kushushwa ,ambapo aliwatuhumu askari polisi kwakuwabambikiza kesi wananchi.
Mwanaume huyo amedai alitaka kufanya hivyo ili kufikisha ujumbe kwa Rais Jakaya Kikwete baada ya kudai kufungwa miaka sita jela kwa kubambikiziwa kesi na polisi.
Mwanzoni alikataa katakata kushuka kutoka katika mnara huo akidai mpaka Rais Kikwete afike eneo hilo aweze kumweleza kero yake hiyo japo wanausalama walifanikiwa kutumia mbinu zao kumshawishi asijirushe na kufanikiwa kushuka naye.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin