Siku chache tu baada ya wanaumme watano kuuawa na wananchi wenye hasira kali kwa kuchomwa moto kwa tuhuma ya kuiba pesa za rambi rambi matukio ya mauaji yameendelea kushika kasi mkoani Geita ambapo usiku wa kuamkia leo mwanamke mmoja ameuawa kwa kuchomwa moto baada ya kutuhumiwa kuiba mfuko wa mahindi maarufu kwa jina “KIROBA”.
Tukio hilo limetokea katika kitongoji cha Ilolangulo
kijiji cha Mbabani kata ya Mtakuja Wilayani Geita ambapo wananchi wamempiga na kumchoma moto mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Savina Sandila mwenye umri kati ya miaka 20-22.
Akizungumzia tukio hilo mmiliki wa shamba la mahindi Milika Migeka alimokutwa marehemu alisema ilikuwa muda wa saa nane na nusu usiku wa kuamkia leo akiwa amelala na mmewe alisikia mtu anavunja mahindi katika shamba lake ambalo liko pembeni mwa nyumba yake.
Amesema mara baada ya kusikia hivyo alitoka nje na kumwona mwanamke huyo (mwizi), akarudi ndani na kumwambia mme wake kilichokuwa kinaendelea shambani kwake.
Amesema baada ya mmewe kutoka nje na kujionea hali halisi ya mtu huyo akiendelea kukata mahindi na aliamua kuita majirani ,wakakusanyika na kumweka chini ya ulinzi kisha kumwambia apige yowe yeye mwenyewe huku akiwa amejitwisha kiroba cha mahindi alichokutwa nacho akipakia tayari kwa kuondoka.
Aidha mwanamke huyo baada ya kuulizwa na wananchi hao kuwa mahindi hayo anayapeleka wapi alisema anaenda kuuza mjini na baada ya kushindwa kupiga yowe wananchi hao walianza kumshambulia kwa mawe na marungu na kumuua papo hapo.
Baada ya kufanya mauaji hayo wananchi walianza kukusanya kuni na kumrundikia juu yake ili wamchome kabisa.
Hata hivyo zoezi la kumchoma moto liligonga mwamba baada ya mwenyekiti cha kitongoji cha Ilolangulo Abeli Kideshe kufika eneo la tukio na kuwazuia ndipo wananchi hao wakaacha na kuondoka eneo la tukio na
kuita jeshi la polisi ambao hata walifika si muda mchache tu kwenye eneo la tukio.
Mwenyekiti wa kitongoji hicho amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi bali wawapeleke kwenye vyombo vya sheria ili haki ikatendeke huko.
Hata hivyo baadhi ya wanachi waliohojiwa na waandishi wa habari waliofika kwenye tukio hilo wameeleza kuwa mama huyo alikuwa mzoefu wa kuiba mahindi kwenye mashamba ya watu na amekuwa akiwatambia vilabuni kuwa yeye hakuna wa kumgusa katika kijiji hicho.
Kamanda wa polisi wa mkoawa Geita Kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Bw Leonard Paul amethibitisa kutokea kwa tukio hili na kueleza kuwa upelelezi na uchunguzi unaendelea ili kuwabaini waliohusika na kitendo hicho ili sheria ichukue hatua.
Na Valence Robert -Geita
Social Plugin