MCHIMBAJI WA MADINI AUAWA KWA KUCHOMWA KISU KIFUANI ,WALIKUWA WANAGOMBANIA MWANAMKE NA MWENZAKE HUKO KAHAMA
Tuesday, January 14, 2014
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangala
Mchimbaji wa madini
aina ya dhahabu aliyejulikana kwa jina
la Emmanuele Chacha(29) ameuawa kwa
kuchomwa kisu kifuani na mwanamme mwenzie katika ugomvi wa kugombea mwanamke
katika kijiji cha Kalole kata ya Lunguya wilayani Kahama katika mkoa wa
Shinyanga.
Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga
SACP Evarist Mangala kwa vyombo vya
habari tukio hilo limetokea Januari 10 mwaka huu saa tano usiku katika
kijiji hicho cha Kalole wilayani Kahama.
Alisema Emmanuel
Chacha ambaye ni mchimbaji mdogo wa madini aina ya dhahabu mkazi Nyangalata wilayani Kahama mwenyeji wa Tarime
mkoani Mara aliuawa kwa kuchomwa kisu
kifuani na mchimbaji mwenzake wa madini
Cosmas Mazigo (23) ambaye ni mkazi wa wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
Kamanda Mangala alikitaja chanzo cha mauaji hayo kuwa ni
ugomvi wa kugombea mwanamke ambay bado
hajafahamika kitendo ambacho kilisababisha marehemu kuchomwa kisu kifuani na
kusababisha kifo chake papo hapo na
mtuhumiwa anashikiliwa kwa hatua
za kisheria.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin