Ikiwa ni siku chache tu
baada ya mtoto Geofry kuibiwa siku ya krismas
aliibiwa akiwa anasubiri wazazi wake kwenda kanisani hali hiyo imejitokeza tena
mara baada ya mtoto mwingine aliyefahamika Peter Shakini (6) mkazi wa Katoro ameibiwa
na kupelekwa kusikojulikana.
Tukio hilo limetokea Desemba 30 mwaka jana baada ya kuchukuliwa na
Majuto Kurwa kwa baiskeli kutoka nyumbani kwa mama yake mzazi aitwaye Semeni
Makoye (25) .
Imeelezwa kuwa baadae mtuhumiwa aliyekuwa amemchukua mtoto huyo
alirudi nyumbani kwa mama huyo akiwa hana mtoto na kumwambia kuwa alitekwa na
watu wanne waliokuwa na gari aina ya Noah asiowafahamu na kupelekwa katika pori
moja la Samina lililopo katika kata ya mtakuja wilayani Geita.
Mtuhumiwa huyo alisema akiwa katika pori aliteswa na baadae alipewa
namba ya simu ambayo alielekezwa ampe mjomba wake aitwaye Maneno Makoye ndipo
mtoto huyo ataachiwa.
Hata hivyo uchunguzi umebaini kuwa mtuhumiwa Majuto Kurwa kabla ya
wizi wa mtoto huyo aliwahi kumfuata mama yake mdogo na kumwambia atembee naye
kimwili lakini siku tu chache baada ya mama yake kukataa ndipo alipomchua mtoto
kwa baiskeli na alirudi kwa mama wa mtoto alidai kuwa ametekwa na watu wenye
gari aina ya noah na kumpora mtoto ambapo taarifa hizo zilitiliwa shaka na
polisi na kumshikilia Majuto Kurwa na katika upelelezi ilibaini kuwa majuto
alimiba mtoto na kumficha na ndipo alipokamatw mtuhumiwa mwenzake Makungu
Panga(28) mkazi wa katoro.
Hata hivyo Majuto alipohojiwa zaidi baada ya kutolewa mahabusu
alieleza kuwa mtoto huyo amefichwa kijiji cha chigunga tarafa ya Butundwe
ambapo mama huyo akienda huko atamkuta hata ingawa hali ya motto huyo baada ya kupimwa alionekana amekutwa na UTI.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Leonard Paul amethibitisha kuwepo
kwa tukio hilo na kuongeza kuwa taratibu za kisheria zimeshaanza ili kubaini
mtandao huo ili ukomeshwe mara moja na ameendelea kutoa wito kwa wananchi kutoa
ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuweza kubaini watu wa namna hii na
kuwachukulia hatua za kisheria.
Na Valence
Robert- Geita
Social Plugin