Aida Nakawala mwenye umri wa miaka 25 kutoka kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya aliejifungua watoto wanne mapacha kwa mkupuo kwenye usiku wa kuamkia Mwaka mpya, anaendelea vizuri.
Watoto hao wanne mapacha |
Muuguzi anasema Watoto hawa walizaliwa wakiwa na uzito uliotofautiana kwa mtoto wa kwanza hadi wa mwisho kuanzia kilo 1.6,1.5,1.5 na 2.0 ambapo baada ya kuona hali hiyo ilibidi kumpa rufaa kwa ajili ya msaada zaidi katika Hospitali ya wazazi ya Meta ambapo waliwekwa kwenye Chumba cha joto.
Anasema watoto wananyonya vizuri na iwapo maziwa yanapungua kwa mama utahitajika msaada wa maziwa ya kopo ili watoto waendelee kupatiwa maziwa kama kawaida.
Bi Aida |
Aida Nakawala alisema hali yake kiuchumi siyo nzuri kuweza kumudu kuwalea watoto hawa kwa sababu mume wake ni mkulima tu hivyo anaomba msaada wa hali na mali kutoka kwa wasamaria wema.Alisema huo ni uzao wake wanne ambapo mtoto wake wa kwanza ana umri wa miaka saba, anaefata ana miaka miwili na miezi tisa ila wa tatu alifariki ambapo alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa hali kama hiyo ya kujifungua watoto zaidi ya mmoja katika familia yao, amesema Mama yake mzazi amewahi kujifungua mapacha wawili tu na hakuna mtu mwingine aliyewahi kuzidisha idadi hiyo ya watoto kama yeye.
credit-Mbeya yetu
Social Plugin