Abiria
17 akiwemo waziri wa katiba na sheria Zanzibar Mhe. Abubakar Khamis Bakar, na marubani wawili, wamesalimika kifo jioni ya leo baada ya ndege ya shirika
la ndege la ‘Zanz air’ kufeli breki, muda mfupi wakati ndege hio ilipo
kuwa ikitua kwenye uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume, uliopo nje
kidogo ya mji wa Chakechake mkoa wa kusini Pemba.
Kwa mujibu wa tarifa zilizo tolewa na makamanda wa
polisi mkoa kusini Pemba kamishina msaidizi swalehe mohamed swalehe na
kamanda wa kikosi cha zima moto na uokozi pemba wamesema ndege hiyo
wakati wa kutua ilipata ikhitilafu ya kufeli breki na kusereka hadi nje
ya uwanja umbali wa mita miambili kwenye vichaka
Wamesema abiria wote wametoka salama hakuna alie
juruhiwa licha ya ndege hio kuacha uwanja kusereka kwenye nyasi na
kungia kwenye mashamba ya muhogo kupita kwenye masiki majiti yalio katwa
nakisha kusimama baada ya ringi kujizonga namizizi ya pori hilo.
Ipo haja kwa mamlaka ya viwanja vya ndege nchini
kutoa taluma kwa watendaji wa kiwanja cha ndege kisiwani pemba kutoa
ushirikiano kwa wandishi wa habari pale inapo tokea dharura kutokana na
watendaji wa kiwanja chandege kisiwani hapa kushindwa kabisa kutoa
usjhirikiano kwa wandishi juu ya tukio hili.
Credit-ITV
Social Plugin