Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Neema yaziangukia shule za Kata Kahama !!! MGODI WA BUZWAGI WATOA SARE ZA SHULE KWA MAMIA YA WANAFUNZI,KUPITIA MRADI WAKE WA CAN EDUCATE ULIOANZISHWA MWAKA 2011



Mapema leo ni katika shule ya sekondari Mwendakulima iliyopo katika kata ya Mwendakulima wilayani Kahama.Wawakilishi wa wanafunzi  200 kutoka shule ya sekondari Mwendakulima  iliyopo katika kata ya Mwendakuli wanafunzi 100 katika shule ya sekondari Nyasubi iliyopo katika kata ya Nyasubi na wanafunzi 100 kutoka shule ya sekondari Bugisha iliyopo katika kata ya Mondo mashati,suruali,sketi na masweta vyenye thamani ya shilingi milioni 15 na laki 2 wakisubiri kupokea sare za shule  kutoka katika mradi wa CAN EDUCATE kupitia  Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu African Barrick katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi.
Katika mwaka 2013 kupitia mradi huo wa CAN EDUCATE wametoa shilingi milioni 43 na laki 6 kufadhili watoto hao mia nne kutoka familia zenye kipato duni,yatima na wale wanaojitahidi katika masomo katika shule hizo kwa kuwasaidia vifaa mbalimbali vya shule pamoja kuwalipia ada.

Awali,aliyesemama ni  mkuu wa shule ya sekondari Mwendakulima ambako zoezi zima la kukabidhi sare hizo limefanyika bi Dianal Kuboja akitambulisha wageni waliohudhuria hafla hiyo fupi kwa ajili ya kukabidhi sare za shule kwa wanafunzi 400 kutoka shule hizo tatu,ambapo pamoja na mambo mengine aliupongeza uongozi wa kampuni ya uchimbaji wa madini African Barrick kwa kuona umuhimu wa kusaidia sekta ya elimu hapa nchini kupitia mradi huo wa CAN EDUCATE.


Wa kwanza kutoka kulia aliyesimama ni afisa mtendaji wa kata ya Mwendakulima bi Cecilia Clement Nekwa akizungumza katika hafla hiyo fupi ambapo amesema mradi huo ni mkombozi mkubwa hasa kwa familia ambazo hazina uwezo wa kusomesha watoto wao lakini pia akatumia fursa hiyo kuwataka wanafunzi hao kutumia misaada wanayopewa kama inavyotakiwa ili kutowavunja moyo wafadhili hao.
Wanafunzi wakisikiliza kilichokuwa kinaendelea katika hafla hiyo,ambapo pamoja na mambo mengine wameaswa kusoma kwa bidii kwani elimu ndiyo mkombozi wa maisha yao na kwamba mgodi wa Buzwagi uko nao bega kwa bega katika kufanikisha malengo yao

Aliyesimama ni meneja wa Kampuni ya African Barrick mahusiano ya jamii bwana Steve Kisyake akizungumza katika hafla hiyo ambapo amesema mradi wa CAN EDUCATE unaendelezwa na kampuni hiyo ya uchimbaji madini ili kuendeleza elimu hapa nchini kwa kushirikiana na kampuni ya uchimbaji madini ya Canada(Canada Barrick) na kwamba mradi huo upo katika kila eneo ambako wanajihusisha na shughuli za uchimbaji madini huko North Mara kuna wanafunzi 200,Bulyanhulu wanafunzi 900 na hapo Buzwagi wanafunzi 400

Baadhi ya sare za shule zilizotolewa leo kwa ajili ya wanafunzi hao 400

Bwana Jesse Audet ambaye ni Coordinator Corporative Social Responsibilities kutoka Toronto akizungumza katika hafla hiyo 

Kulia ni mwakilishi wa wanafunzi  Rachel Mtwale akisoma risala ,ambapo amesema wanafunzi hao 400 wakiwemo  wasichana 185 na wavulana 215 wameahidi kutumia vifaa walivyopatiwa na kwamba watajitahidi kusoma kwa bidii ili wanainua kiwango cha elimu katika shule zao na taifa kwa ujumla.

Meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi bwana Philbert Rweyemamu akikabidhi sare hizo za shule  kwa wanafunzi kutoka shule hizo tatu za sekondari
Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa  Buzwagi uliopo Kahama bwana Philbert Rweyemamuamesema lengo la mradi huo ambao umeanzishwa mwaka 2011  ni kuinua kiwango cha elimu katika shule zote zinazozungukwa na kampuni hiyo ya uchimbaji migodi ambapo katika wilaya ya Kahama unatekelezwa katika shule hizo tatu.


Hafla inaendelea ambapo katika mwaka 2013 kupitia mradi huo wa CAN EDUCATE wametoa shilingi milioni 43 na laki 6 kufadhili watoto hao mia nne kutoka familia zenye kipato duni,yatima na wale wanaojitahidi katika masomo katika shule hizo kwa kuwasaidia vifaa mbalimbali vya shule pamoja kuwalipia ada.

Aliyesimama ni mkurugenzi wa bodi ya ufadhili katika mradi huo bi Catrine White amezipongeza shule wanazozifadhili tangu mradi huo uanze kwa kufanya vizuri katika mitihani na kuongeza kuwa wataendelea kuzisaidia kwani elimu ndiyo njia pekee ya kuondoa umaskini katika jamii.

Picha ya pamoja baada ya zoezi la kukabidhi sare hizo kukamilika katika eneo la shule ya sekondari Mwendakulima iliyopo wilayani Kahama

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com