Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Noma sana!!! MCHAWI ADONDOKA AKIWA KATIKA SAFARI ZAKE WILAYANI KAHAMA



Kikongwe huyo akiwa chini huku amezingirwa na kundi la wananchi

Kikongwe mwenye umri kati ya miaka 85 hadi 90 ambaye bado hajafahamika jina lake amekutwa katika kijiji cha Nyashimbi kata ya Muhongolo wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kwa kile kinachodaiwa kuwa huenda ni mchawi aliyeanguka usiku wakati akiwa kwenyesafari zake angani.


Kikongwe huyo baada ya kufikishwa kituo cha polisi

Kwa mujibu wa wakaazi wa Kijiji hicho bibi huyo ameonekana leo majira ya saa 12 asubuhi akiwa katika vichaka vilivyo kando ya barabara na alipoulizwa aliongea kidogo tu kuwa anatoka Kijiji cha Nyihogo wilayani Kahama.

Alipoendelea kuhojiwa alisema alikuwa na wenzake na vitu mbalimbali ila wamemuacha, huku akisema hawezi kuongea zaidi kwani anahisi njaa kwakuwa alikula toka jana tena chakula Kibichi, jibu ambalo liliwashangaza wengi ni aina gani ya chakula ambacho huliwa kikiwa kibichi.

Bibi huyo amekutwa na nguo moja ya Kimasai na nguo zingine chache za kawaida lakini hakukutwa na vitu vyovyote vinavyoashiria kuwa huenda ni mchawi, hivyo kuleta hisia kuwa huenda alikuwa ni mtembea kwa miguu tu aliyepotea njia kwani watu wote wa eneo hilo hakuna anayemtambua.
Credit-Dunia Kiganjani blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com