SHINYANGA WAZINDUA BODI YA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA
Friday, January 31, 2014
Mapema leo akizungumza katika uzinduzi wa bodi ya hospitali ya rufaa ya mkoa katika ukumbi wa ofisi ya
mkuu wa mkoa mjini Shinyanga kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Dkt Ramadhani Kabala ambapo alisema kuundwa kwa bodi hiyo ni kuleta mabadiliko katika huduma za
hospitali ikiwa ni sehemu ya mabadiliko endelevu katika sekta ya afya chini ya
mkakati wa pili.
Dkt
Kabala alisema lengo la mkakati huo ni kuimarisha uwezo wa hospitali za mkoa na
kanda ili ziweze kutoa huduma bora za rufaa itolewayo na wizara ya afya
na ustawi wa jamii chini ya usimamizi wa bodi zenye uwakilishi wa jamii.
Watu mbalimbali waliohudhuria shughuli ya uzinduzi wa bodi hiyo wakisikiliza hotuba ya Dkt Kabala kabla ya kumkaribisha mkuu wa mkoa wa Shinyang aliyekuwa mgeni rasmi,ambapo Dkt Kabala alisema miongoni maeneo ambayo yanayohitaji mabadiliko ni pamoja na kutotosheleza kwa wataalam
mbalimbali katika hospitali kutokana na hospitali nyingi kukosa uwezo wa kutoa
huduma zote za matibabu kwa kiasi kinachostahili kutolewa.
Eneo jingine ni kukosekana kwa motisha,kushuka ari
na mtazamo mbaya watoa huduma kwa wagonjwa kushuka kwa kiwango na kukosekana
kwa udhibiti wa ubora wa huduma,uchakavu wa vifaa,vifaa tiba,miundombinu na
magari
Mkuu wa mkoa
wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akizungumza wakati akizindua bodi ya hospitali ya rufaa
ya mkoa katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa mjini Shinyanga,ambapo alisema endapo suala la afya likipewa kipaumbele litasaidia katika kuondoa umaskini
katika jamii kwani wananchi watajihusisha na shughuli za maendeleo kutokana
na kwamba afya zao ni nzuri.
Alisema anaamini kabisa kwamba bodi hiyo inayoundwa na wajumbe 17
itakuwa mwakilishi mzuri wa wananchi na kutoa rai kwao wafanye kazi kwa
kuzingatia sheria na taratibu za nchi,na kwamba wahakikishe wanafanya vikao mara
kwa mara yaani kila baada ya miezi mitatu na wafanye kazi kwa uhakika
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa bodi hiyo
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin