Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Tahadhari!!!! UTAPELI MPYA WA FEDHA WAIBUKA,SOMA ZAIDI HAPA

 
Tahadhari kuhusu mbinu mpya ya kutapeliwa fedha ukitoka kwenye ATM

Matapeli wamebuni mbinu mpya ya kuibia watu fedha punde wanapotoka kuzichukua kwenye ATM MASHINE.

Punde unapomaliza kuchukua fedha, anakuja mtu anakuomba msaada wa chenji kwa kuwa naye amechukua fedha ila imempa noti kubwa tu.

Huruma na wema wako wa kutoa chenji unasababisha akupe noti zisizo halali (fake bills) na wewe unakuwa ulishampatia zilizo halali.

Tukio halisi hivi karibuni  lilimtokea mtu ambaye ameamua kuwashirikisha wengine ili wajihadhari.

Alikumbwa na utapeli huo alipochukua fedha katika maeneo ya CBE, Dar es Salaam.

Jihadhari!

Via wavuti.com

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com