Mtoto mmoja wa mwenye umri wa miaka 12 mkazi wa kijiji cha Mwendakulima
kata ya Butengo na tarafa ya Buseresere wilayani Chato mkonai Geita amejeruhiwa
kwa kutobolewa tumboni na kitu chenye ncha kali na Baba yake wa kambo
aliyefahamika kwa jina la Sesa Charles.
Tukio hilo limetokea Januari 19 mwaka huu kijijini hapo ambapo
kijana huyo Amosi Julius Mayila(12) alipata mkasa huo kutoka kwa baba huyo mara
baada ya kutuhumiwa kuficha mafuta ya kujipaka na hadi sasa kijana huyo
amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Geita kwa matibabu zaidi.
Akisimulia kuhusu tukio hilo mama wa mtoto anayemuuguza katika hospitali ya
wilaya ya Geita wodi namba 8 Bi Anastazia Sanyenge(39) alisema kuwa yeye
alikuwa ameenda kwenye sherehe ya harusi kijiji jirani cha Bumba siku ya ijumaa
na wake wenzake 2 kwani mme wao ana wanawake 3 na ndipo siku ya jumapili aliporudi
nyumbani na kukuta watu wengi na mmewe akiwa amekimbia.
Naye jirani yake aliyemsaidia kumpeleka hospitalini Bw Benedict
Faustine alisema kuwa akiwa nyumbani alifuatwa na watoto wakimwambia mwenzao
ameanguka mtini na kuangukia kisiki lakini alipoenda nyumbani akakuta kijana
amepigwa na utumbo umetoka nje na wakaanza kutoa msaada wa kumpeleka hospitali
alipolazwa hadi sasa hivi.
Kwa upande wa mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Geita Bw
Adamu Sijaona alisema kuwa walimpokea motto huyo mnamo saa 7 siku hiyo usiku
akiwa na hali mbaya sana utumbo ukiwa nje na kulazimika madaktari watatu wamfanyie
upasuaji na kumshona hali na kwamba hali yake sasa inaendelea vizuri
Kamanda wa polisi mkoani hapa Kamishina msaidizi mwandamizi Bw,
Leonard Paul amethibitisha kutokea kwa tukio na kueleza kusikitishwa na kitendo
cha Baba huyo wa kambo kutenda kitendo cha kinyama namna hiyo katika jamii.
Kamanda amesema hadi sasa
hivi mtuhumiwa anatafutwa na jeshi la polisi popote alipo ili sheria ichukue
mkondo wake kwani amekimbia baada ya kutenda unyama huo.
Naye katibu wa Kituo cha kutetea haki za Binadamu wilayani hapa Bw
Elineema Charles aliyeenda hospitali kumjulia hali kijana huyo amelaani sana
kitendo hiki kilichofanywa na mtu mzima mwenye akili timamu na kuongeza kuwa
adhabu kwa watoto zipo zinafahamika na si unyama wa aina .
Ameviomba vyombo vya sheria kwa kushirikiana na kamanda wa polisi
huyo wa Geita kwani anaamini atapatikana tuili sheria ichukue mkondo wake.
Na Valence Robert- Geita
Social Plugin