Maisha
ya mwanafunzi wa kike mwenye umri wa miaka 12, (jina tunalihifadhi), anayesoma
darasa la tano Shule ya Msingi Bwanza, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, yako
hatarini baada ya kurukiwa na samaki aina ya sato, kuingia sehemu ya siri na
kukimbilia tumbani.
Tukio
hilo limetokea Januari mosi mwaka huu, saa 11 alfajiri,wakati mtoto huyo akichota maji katika Ziwa Victoria ili aweze kumwagilia bustani ya
nyanya, vitunguu iliyopokandokando ya ziwa hilo.
Kaka wa mtoto huyo (jina tunalihifadi), mwenye miaka
31, alisema tukio hilo limewashangaza wakazi wa Kijiji cha Bwanza na vitongoji
vyake.
Alisema mdogo wake alikuwa akichota maji katika ziwa
hilo akiwa amechuchumaa ndipo samaki huyo anayedaiwa kuwa mwenye ukubwa wa nchi
nne, aliruka kutoka majini, kuingia sehemu yake ya siri na kukimbilia tumboni.
"Mdogo
wangu alifanya jitihada za kumvuta ili aweze kumtoa lakini alikimbilia tumboni
na kuanza kupata maumivu makali,kutokwa na damu nyingi baada ya kuparazwa na
miba ya
mgongo wa samaki huyo.
mgongo wa samaki huyo.
"Baada
ya tukio hilo, alirudi nyumbani kwa shida akijivuta na kuugulia
maumivu...alimweleza mama na ndugu zake juu ya mkasa huu, walimchunguza na
kujaribu kuingiza mkono sehemu za siri wakidhani watampata lakini
hawakufanikiwa," alisema.
Aliongeza
kuwa, baada ya kumpeleka zahanati iliyopo kijijini hapo, hali yake ilizidi kuwa
mbaya akilalamika maumivu makali tumboni ambapo familia inaamini tukio hili
limetokana na imani za kishirikina hivyo waliamua kumtoa katika zahanati hiyo.
"Tulimpeleka
kwa mganga wa kienyeji kijiji cha Amuyebe,wilayani Ukerewe...katika hali ya
kawaida samaki hawezi kumrukia mtu sehemu yake ya siri na kuzama tumboni.
"Pamoja
na kuchukua uamuzi wa kumpeleka kwa mtaalamu,hali yake bado inazidi kuwa mbaya,
hata baba yetu alifariki katika mazingira yenye utata mwaka 2003,"
alisema.
Aliongeza
kuwa, hata kaka zake watatu na mtoto huyo nao walifariki kwa mfululizo mwaka
2004, 2005, 2006 ambao vifo vyao viligubikwa na utata mkubwa.
Mwenyekiti
wa Kitongoji cha Alwego anakoishi mtoto huyo, Bi. Reticia Bituro, alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo ambalo limewashangaza watu na kuahidi uongozi wa
kitongoji hicho utaendelea kufanya uchunguzi zaidi.
Diwani
wa Kata ya Napindi, Bw. Elias Magoti ambaye yuko safari kuhudhuria kikao cha
Baraza la Madiwani Bunda Mjini,alikiri kupokea taarifa za tukio hilo kwa
mshangao mkubwa.
"Nitalifuatilia
kwa karibu baada ya kurudi kijijini kwa kufanya uchunguzi ili kubaini
kilichotokea kwani sijawahi kusikia tukio kama hili katika umri nilionao,"
alisema.
Taarifa
zilizopatikana kutoka Ukerewe anakotibiwa mtoto huyo, zilisema kwa sasa hawezi
kuzungumza akizidi kulalamika maumivu makali ya tumbo na samaki huyo bado
hajatolewa.
Credit-MAJIRA.
Social Plugin