Kwa mara
kwanza umoja wa vijana wa CCM ( UVCCM) wilaya ya Shinyanga mjini umeadhimisha
sherehe za kutimiza miaka 37 ya Chama cha mapinduzi CCM katika kituo cha watoto
wenye ulemavu wa ngozi cha Buhangija
jumuishi kilichopo mjini hapa kwa
kufanya usafi pamoja katika kituo hicho
samabamba na kutoa msaada wa vyakula.
Umoja huo umetoa kilo hamsini za mchele pamoja na mafuta ya kupikia lita
kumi vyote vikiwa na thamani ya shilingi elfu themanini na saba pamoja na
kupanda miti 30 ya matunda na kivuli katika kituo hicho hapo jana
Mwenyekiti wa umoja huo bwana Abubakari Mkadam amesema wameona vyema kuadhimisha
sherehe hizo za miaka 37 ya CCM kwa kutembelea katika kituo hicho cha walemavu
wa ngozi kwa kufanya usafi wa mazingira, kupanda miti kufua nguo pamoja na
kugawa chakula ,kwa lengo la kushiriki nao sherehe hizo za kuzaliwa kwa CCM na
kwamba sherehe nyingi za CCM zimekuwa zikiadhimishwa kwa kufanya mikutano
mbalimbali ya wananchi lakini kwa mwaka
huu (2014) wao wameona wafanye tofauti
kwa kuwatembelea vijana wenzao ambao huishi katika mazingira magumu na
hatarishi.
Hata hivyo mkuu wa kituo hicho cha
walemavu Briton Mduma amezitaja changamoto kubwa zinazowakabili vijana hao
walemavu kuwa ni uhaba wa chakula, vifaa vya kufanyia usafi ,vyandarua, pamoja
na upungufu wa vitanda ambapo kuna watoto 258 huku kukiwa na vitanda 60 na kuwa
lazimu kulala wane wane hadi watano katika kitanda kimoja.
Naye mmoja wa watoto hao wenye
ulemavu ngozi katika kituo hicho Semen Deus amewashukuru vijana hao wa UVCCM
kuwatembela katika kituo hicho na kukishukuru chama tawala kwa kuwakumbuka
katika siku za maadhimisho yake huku akitoa wito kwa vyama vingine kuiga mfano
huo .
Social Plugin