Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZAZI WAJITOA MHANGA ,WACHANGIA MADAWATI SHULE KONGWE YA BUGOYI A ILIYOPO MJINI SHINYANGA

Mapema leo madawati  25 kati ya 72 yanayotokana na mchango wa wazazi na walezi wa wanafunzi 1200  wanaosoma katika shule ya msingi Bugoyo A iliyopo mjini Shinyanga yakishushwa kwenye mkokoteni huku wanafunzi wakionesha hali ya furaha kutokana na kuondokana na hali ya kukaa chini ilihali shule iko mjini Shinyanga

Kushoto ni mwenyekiti wa kamati ya shule ya Bugoyi A  bwana Peter Sangwa akikabidhi madawati hayo kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo hiyo Selemani Shaban Kipanya (aliyejishika kiuno kulia) amesema kupitia vikao na mikutano mbalimbali na wazazi hao walikubalina kila mzazi achangie  kiasi cha shilingi elfu kumi kwa kila mtoto na kwamba michango hiyo ilianza tangu Julai mwaka 2012.Lengo lao ni kupata madawati 100,katika awamu ya kwanza wazazi walichangia madawati 47 na kila dawati likiwa na thamani ya shilingi elfu 70  na katika mwezi Desemba 2013 na Januari 2014 wazazi  wamechangia madawati 25 kila dawati likiwa na gharama ya shilingi elfu themanini.
 Wazazi na walezi hao wamechangia madawati 72 yenye thamani ya shilingi 5,290,000/= ili kukabiliana na changamoto ya wanafunzi hao kukaa chini pamoja na kwamba shule hiyo iko mjini
Kulia ni mwalimu mkuu wa Shule Selemani Shaban Kipanya,wa pili kutoka kulia ni mwenyekiti wa mtaa wa Mbuyuni ilipo shule hiyo bwana Chifu Abdalah Sube,wa tatu ni mwenyekiti wa kamati ya shule ya Bugoyi A  bwana Peter Sangwa ,wa kwanza kutoka kulia ni mwandishi wa habari radio Faraja bwana Marco Maduhu wakiangalia madawati hayo.
Pamoja na kupata madawati hayo 72 shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 1200,wavulana wakiwa ni 650 na wasichana 550 na walimu 27 wawili kati yao ni wanaumme lakini  bado ina upungufu wa madawati 28.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com