Watanzania wengi hasa wafuasi na wapenzi wa CHADEMA macho na masikio yao yalikuwa yameelekezwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,pale ambapo Jaji wa Mahakama hiyo Jaji John Utumwa alikuwa akitoa hukumu dhidi ya Zitto Kabwe na CHADEMA....
Zitto ambaye alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, alifungua kesi katika Mahakama hiyo akipinga hatua ya Kamati Kuu ya Chama hicho iliyokutana tarehe 3 na 4 mwezi huu kujadili hatima ya uanachama wake wakati baraza kuu halijakaa na kujadili rufaa yake...
Akisoma hukumu ya kesi hiyo baada ya kuiahirisha jana, Jaji wa mahakama hiyo,Jaji Utamwa ameridhia pingamizi lililotolewa na mh. Zitto Kabwe la kutojadili uanachama wake na kuitaka kamati kuu ya CHADEMA au chombo kingine chochote kisijadili uanachama wake hadi kesi yake ya msingi ( rufaa ) itakaposikilizwa na baraza kuu la chama hicho.
Social Plugin