NB picha haiendani na tukio la ajali ya leo
Bus kampuni ya Zubery
lenye namba za usajili T 119 AZZ lililokuwa likitokea jijini Mwanza kwenda
jijini Dar es salaa , limepinduka leo majira ya saa 7 mchana wa leo eneo la
Isuna wilaya ya Ikungi mkoani SINGIDA na mpaka sasa taarifa tulizonazo ni kwamba takribani watu 2 kati ya 60 waliokuwemo ndani ya basi hilo wameripotiwa kufariki dunia papo hapo
eneo la tukio.
Habari kutoka eneo la
tukio zinasema kuwa chanzo cha ajali
hiyo ni baada ya basi hilo kutaka kumkwepa bibi kizee aliyekuwa anakatiza
barabara ndipo lilipopinduka.
Walioshuhudia tukio hilo wamesema ajali hiyo imehusishwa na imani za kishirikina kutokana na kile kilichodaiwa kuwa baada ya ajali hiyo bibi huyo alirudi nyuma mara ya pili na kusababisha ajali hiyo kisha kukaa kwa muda mrefu katika eneo la tukio.
|
Social Plugin