Askari polisi akipanda juu ya mti ili akate kamba aliyotumia marehemu kujinyonga |
Askari akiendelea na shughuli ya kushusha mwili wa marehemu |
Marehemu akiwa juu ya mti |
Mwili wa marehemu ukichukuliwa kutoka eneo la tukio na kupelekwa hospitali ya mkoa wa Kagera |
Mwanamme mmoja aliyejulikana kwa jina moja Bahati amabaye
hujishughilisha na uuzaji wa mifuko ya plastiki katika stendi kuu ya mabasi
mjini Bukoba amekutwa amejinyonga juu ya mti katika eneo ufukwe wa Spice Beach Motel leo majira ya saa nane mchana.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema kabla ya kifo cha marehemu
walimwona jamaa huyo akiwa na mafurushi ya vitu mbalimbali na alikuwa nafua
katika eneo hilo la Beach ya Spice Motel mjini Bukoba .
Aidha taarifa za awali zinasema kuwa mapema leo asubuhi
mwanamme huyo maarufu kwa uuzaji wa mifuko ya plastiki alionekana katika eneo
la stendi kuu ya mabasi Bukoba akiuza mifuko hiyo kwa wasafiri waendao mikoani.
Mwili wa marehemu umepelekwa katika hospitali ya Mkoa wa
Kagera kuhifadhiwa kwa ajili ya ndugu wa marehemu kuutambua mwili wa marehemu.
Social Plugin