Breaking News!!! BASI LA BUNDA EXPRESS LAGONGA TRENI HUKO SINGIDA
Friday, February 28, 2014
Eneo la tukio
Habari kutoka Manyoni mkoani Singida zinasema kuwa Basi
la Bunda Express lililokuwa linatoka Dodoma kuelekea Mwanza limegonga Treni iliyokuwa inatoka Aghondi Itigi katika eneo la njia panda ya Itigi Na Singida.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka eneo la tukiokinasema kuwa mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Bi Kombo amefariki dunia na kadhaa kujeruhiwa. Majeruhi 38 tayari wamepelekwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Manyoni. Chanzo cha ajali inasemekana kuwa ni uzembe wa dereva ambapo inadaiwa dereva wa gari hakusimama wakati anajua anapaswa kusimama katika eneo hilo la njia ya treni.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin