Habari tulizozipata hivi punde kutoka Bunda mkoani Mara mwandishi wa gazeti la Mwananchi Christopher Maregesi amepigwa kisha kuporwa vifaa vyake vya kazi na wafuasi wa CCM
Imeelezwa kuwa chanzo cha tukio hilo wanadai kwanini alipiga picha wakati vijana wao wakimshambulia mtu aliyedaiwa kuwa mfuasi wa Chadema baada kuisha kwa kampeni za uchaguzi mdogo wa kata ya Nyansura.
Kwa mujibu wa mwandishi George Marato aliyeko Bunda Chama cha waandishi mkoani Mara (MRPC) kimelaani kitendo hicho na kutoa siku saba kwa CCM kuomba radhi,kurejesha vifaa vya kazi vya mwandishi huyo na kutoa fedha za matibabu la sivyo waandishi wote wa mkoa wa Mara watasusia kuandika habari za CCM........
Habari zaidi endelea kufuatilia hapa malunde1 blog
Social Plugin