Madiwani
wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Cchadema) katika
manispaa ya Shinyanga wametanganza rasmi kujiuzulu nyadhifa zo kutokana na
madai ya uongozi ngazi ya taifa kuendelea kusikiliza majungu,kudhalilisha
baadhi ya viongozi pamoja na kuwaita wahaini au wasaliti
katika chama bila kuchambua ukweli na kutotekeleza waliyoyaahidi kwa
wanachama wao.
Madiwani hao
ni Sebastiani Peter (PICHANI) kutoka kata ya Ngokolo na Zacharia Mfuko kutoka kata
ya Masekelo ambao wamedai wanayatamka rasmi
maneno mbalimbali yaliyopelekea kujiuzulu kama inshara ya kuwajibika kwa
niaba ya makosa yaliyofanywa na viongozi wa chama hicho kitaifa kwa nyakati tofauti.
Social Plugin