Wafuasi wa CCM kata ya Nduli wakiwa wamemnyanyua juu juu aliyekuwa mgombea udiwani kata ya Nduli Bw Mtove baada ya matokeo kumpa ushindi wa kishindo leo
CHAMA cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kimefanikiwa kutetea kata zake zote tatu ambazo leo wananchi wameshiriki kupiga kura kuwachagua madiwani kufuatia nafasi hiyo kuwa wazi baada ya madiwani wake kufariki dunia huku chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) kikishindwa vibaya katika uchaguzi huo.
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (Chadema) ambae alikuwepo eneo la Nduli akifuatilia matokeo ya uchaguzi huo pamoja na wafuasi wa Chadema alilazimika kuondoka katika eneo hilo baada ya kubaini kuwa hali ya ushindi kwa Chadema ni ndoto.
Huku wafuasia wa CCM wakionekana kumpongeza aliyekuwa mgombea wa CCM kata ya Nduli pamoja na kaimu katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga kuwa kazi yake imeonyesha inaonyesha wazi safari yake ya kulitwaa jimbo la Iringa mjini .
Katika Matokeo hayo ambayo hadi sasa majira ya saa 12.50 bado msimamizi wa uchaguzi kutangaza CCM inaongoza kwa kura 810 huku Chadema wakifuatia kwa kura 491
Mbali ya matokeo hayo ya kata ya Nduli pia CCM imeshinda kata ya Ibumi na Ukumbi zote za wilaya ya Kilolo.
Na Francis Godwin
Social Plugin