Kufuatia Chama Cha Mapinduzi kupata ushindi katika uchaguzi wa diwani katika
Kata ya Ubagwe wilayani Kahama mkoani Shinyanga chama hicho kimewapongeza wakazi wa kata hiyo kwa uamuzi
wao wa busara wa kumchagua diwani anayetokana na chama hicho bwana Hamis Majogor hali ambayo inaonesha bado
wana imani na mapenzi makubwa kwa CCM.
Pongezi
hizo zimetolewa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja alipokuwa
akiwahutubia wananchi wa Ubagwe ambapo Mgeja alisema wakazi wa kata hiyo wameonesha
kwa uwazi mpana kwamba bado wana imani kubwa na CCM ambapo pamoja na vurugu na
vitisho vya wagombea wa vyama vya upinzani hasa CHADEMA, ambapo baadhi ya
wafuasi wa CCM walicharangwa mapanga lakini bado wananchi wamemchagua diwani wa CCM.
Mgeja
amesema CCM hivi sasa ndiyo iliyosalia na deni kubwa kwa wakazi wa kata ya
Ubagwe na wilaya ya Kahama kwa ujumla ya kuhakikisha kwamba inawaondolea kero
mbalimbali ambazo iliahidi kuzifanyia kazi na kwamba moja ya vipaumbele vya
serikali ya CCM kwa hivi sasa ni kilimo, afya, elimu na upatikanaji wa maji
safi na salama.
Social Plugin