Mwanamke wa nchini Uingereza ambaye alishawahi kufikishwa mahakamani kutokana na makelele yake ya kimahaba anayoyatoa wakati akifanya mapenzi na mumewe ametiwa tena mbaroni kwa mara nyingine baada ya kuwasumbua tena majirani zake kwa kelele zake za ngono.
Caroline Cartwright alifikishwa mahakamani wiki nane zilizopita kwa kuvunja amri ya mahakama ya kutowasumbua tena majirani zake kwa kelele zake za ngono anapofanya mapenzi na mumewe, Steve. Caroline mwenye umri wa miaka 49 alihukumiwa kifungo cha nje wakati huo na kuamuriwa aache kupiga kelele wakati wa tendo la ndoa na mumewe.
Lakini wiki iliyopita Caroline alitiwa tena mbaroni kwa kuwasumbua majirani zake na kelele za ngono kwenye majira ya saa nne asubuhi ya siku ya jumapili.
"Ilikuwa ni dakika 10 tu sio masaa mawili kama kawaida yetu, iweje majirani wametusikia wakati kitanda tulikiamshia chumba cha chini na sio chumbani", alilalamika Caroline.
Mwaka jana Caroline kutokana na kosa kama hili alihukumiwa kifungo cha nje cha miezi 12 na kuamuriwa asitoe kelele tena wakati akifanya mapenzi kwenye maeneo yoyote ya nchini Uingereza na Wales.
Mahakama ilisikilizishwa sauti anazotoa bi Caroline Cartwright wakati akifanya mapenzi na mumewe Steve Cartwright na kuungana na madai ya majirani wa mtaa wake ambao walisema kuwa kelele zake huwakosesha usingizi kwani ni sawa na kelele za mtu aliyekuwa kwenye maumivu makali sana wakati akijeruhiwa au kutolewa roho.
Ilidaiwa pia kuwa hata jirani yake mmoja ambaye ni nusu kiziwi hukosoka usingizi kelele hizo zinapoanza.
"Sauti anazotoa Caroline na miungurumo ya mumewe Steve si za asili ni kama vile wote wawili wapo kwenye maumivu makali sana", mahakama iliambiwa katika kesi yake ya awali.
Caroline atafikishwa tena mahakamani mei 13.
Social Plugin