Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani
Shinaynga kimepata pigo kubwa baada ya madiwani wake wawili katika manispaa ya
Shinyanga kutangaza kujiuzulu nyadhifa zao kutokana na madai kuwa viongozi ngazi ya taifa wa chama hicho
kundekeza majungu,migogoro ,kudhalilisha
baadhi ya viongozi pamoja na kuwapa majina ya wasaliti wa chama.
Madiwani waliofikia
maamuzi hayo magumu ni diwani wa Kata ya Ngokolo Sebastian Peter maarufu
OBAMA WA NGOKOLO na Zacharia Mfuko wa kata ya Masekelo ambao wamesema wameamua kufikia maamuzi hayo magumu
kama ishara ya kuwajibika kwa niaba ya makosa yaliyofanywa na viongozi wa chama
hicho kitaifa.
Madiwani hao wawili tayari wameshakabidhi barua za kung’atuka
nafasi zao katika ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga
Hili ndiyo barua ya tamko la diwani wa Ngokolo Sebastian
Peter kuhusu kujiuzulu nafasi yake ya udiwani aliyoikabidhi ofisi ya
mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga ikielez sababu za kuchukua maamuzi hayo
huku akisisitiza kuwa atabaki kuwa mwanachama mwadilifu wa Chadema
|
Social Plugin