NB-Picha haihusiani na tukio katika habari |
Mwalimu wa shule ya msingi Mwang’osha kata ya Nyamalongo wilaya ya Shinyanga Vijijini Christipian Mafuru (24) amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani katika choo kilichopo nyumbani kwake.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwalimu mkuu wa shule hiyo Frida Maleko amesema marehemu Mafuru amegundulika akiwa amejinyonga juzi majira ya saa tisa na nusu alasiri.
Amesema baada ya mwalimu huyo kutoonekana shuleni hapo kwa muda mrefu walijaribu kumpigia simu marehemu bila mafanikio na kuamua kuondoka na walimu wenzake kwenda nyumbani kwake na kukuta mlango umefungwa huku simu ikiita ndani bila ya kupokelewa.
Maleko amesema walichukua jukumu la kuvunja dirisha na mara baada ya kufanikiwa kuingia ndani walikuta ujumbe wa maneno mezani uliokuwa umeandikwa na marehemu ukisomeka kuwa.......
"MSONGO WA MAWAZO UMENILAZIMU NIFANYE HIVI,POLENI SANA WALIMU WENZANGU,SAMAHANI WAZAZI WANGU,KWA HERI MWANANGU REY"
Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Evarist Mangalla amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Social Plugin