Katika hali ya kusikitisha mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Christina Charles
(20) mkazi wa Kharumwa mkoani Geita amefariki
dunia akiwa Guest(Nyumba ya kulala wageni) akiwa na mpenzi wake Mniry Masii mfanyakazi
wa kituo cha afya cha Kharumwa katika halmashauri ya wilaya Nyang’hwale mkoani
Geita.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana katika
Nyumba ya kulala wageni iliyopo mjini Nyang’wale inayojulikana kwa jina
la Saju Guest house.
Imedaiwa kuwa siku hiyo mtuhumiwa ambaye ni mfanyakazi
wa kituo hicho cha afya ambaye ni katibu
wa kituo cha afya Kharumwa anayefahamika kwa jina la Mniry Masii
alimchukua Christina Charles(20) ambaye ni mkulima muda wa saa tatu usiku na kwenda
naye katika gesti hiyo na kupewa chumba kwa ajili ya kupumzika.
Habari zinasema kuwa ilipofika saa 7 usiku mhudumu wa gesti hiyo
aliitwa na (Mniry Masii) mtuhumiwa huyo aende kwenye chumba chake na alipofika
alimkuta huyo mama anatoa mapofu na mtuhumiwa akiwa amekaa pembeni huku akilia....
Mhudumu
alipomuuliza mwanamme(Mniry Masii) kulikoni!! ,hakujibu chochote zaidi
ya kuendelea kulia kutokana na kutojibiwa yule mhudumu alirudi alikokuwa.
Imeelezwa kuwa mhudumu huyo wa gesti aliporudi
na kulala baada ya muda mfupi tena akaitwa tena na bwana Mniry Masii
akasema kuwa mpenzi wake Christina amebanwa na kifua ,ndipo wakambeba na
kumpeleka hospitali ya Kharumwa na walipofika tayari alikuwa amefariki dunia.
Diwani wa kata ya Kharumwa Marco Masusu amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa tayari mazishi yameshafanyika.
Hata hivyo inadaiwa kuwa mwanamke huyo enzi za
uhai wake alikuwa na matatizo ya kuugua kifua na baadhi ya watu wamesema kuwa
huenda hali ya hewa kulingana na tatizo hilo imepelekea kuweza kupoteza maisha
katika hali aliyokutwa nayo.
Naye mama mzazi wa marehemu Bi, Salome Nkuji (30)
ambaye ni mkazi wa Mwanza alipofika msibani alieleza kuwa binti yake
alikuwa na matatizo ya muda mrefu tangu azaliwe.
“ Binti yangu tangu nimzae miaka 20 iliyopita alikuwa
na tatizo la kifua (athma)’’ ,alisema mama huyo bila ya kuongeza lolote.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani Geita Simon Pasua
amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kuongeza kuwa Mniry Masii (mtuhumiwa )
hajatenda kosa la kuua bali ni hali ambayo imetokea kama ambavyo mtu anaweza
kuwa amelala na mtu mgonjwa halafu mauti yakampata .
“Ndugu mwandishi ni kweli tukio lipo lakini haya sio
mauaji ni mtu ambaye alikuwa anaumwa
siku zake zimefika kwa hali hiyo na tulimshikilia mtuhumiwa tumemhoji na tayari
tumeshamwachia”,alisema kamanda Pasua.
Na Valence Robert-Geita
Social Plugin