Baadhi
ya watu waliokwama kijiji cha Fulwe kata ya Mikese mkoani Morogoro
wakiangalia mwili wa dereva wa lori lililobeba shehena ya mafuta
lililokuwa likitoka Dar kueleka upande wa Morogoro, ukiwa umeteketea
vibaya kwa moto baada ya ajali.
Mwili Mwili wa dereva wa lori la mafuta ukiwa umeteketea kwa moto.
Lori la mafuta baada ya kuteketea kwa moto kijiji cha Fulwe, Mikese mkoani Morogoro. |
AJALI hii imetokea leo katika kijiji cha Fulwe, kata ya Mikese mkoani
Morogoro ambapo malori mawili yamegongana na kuteketea kwa moto.
Katika ajali hiyo, dereva wa lori moja lililokuwa na shehena ya
mafuta amepoteza maisha wakati dereva wa lori lingine aina ya semitrela
akijeruhiwa pamoja na tingo wake na kukimbizwa hospitali.
Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo amedai kuwa dereva aliyepoteza
maisha alishindwa kujiokoa baada ya ajali kutokea kwa kubanwa hali
iliyopelekea kuungua vibaya kwa moto.
"Lori hili la mafuta lilikuwa likitoka Dar na kushuka mteremeko huu
kwa kasi huku semitrela likijaribu kulipita lori lingine eneo hili hivyo
kugongana uso kwa na lori la mafuta.
Baada ya kugongana, mafuta yaliokuwa kwenye tenki yalimwagika hali
iliyosababisha malori yote kuteketea kwa moto. " Alisema shuhuda huyo
mkazi wa kijiji cha Fulwe, Bw Issa Athuman.
Credit-GPL
Social Plugin