Kilio cha wasanii kuitaka katiba mpya kuitambua sanaa ya
Tanzania kama sekta rasmi kimepewa sapoti na Naibu waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January makamba na mbunge wa Mbeya
Mjini Joseph Mbilinyi aka Sugu.
Kwa mujibu wa mtandao wa Bongo5, Makamba na Sugu wameshiriki kwenye
wimbo wa hip hop uliowahusisha rappers 13 wa Tanzania, wimbo wenye lengo
la kusisitiza sanaa kutambulika kwenye katiba mpya. Katika wimbo huo,
January Makamba amefanya Intro na Outro imefanywa na Sugu.
Rappers walioshiriki kwenye wimbo huo uliopewa jina la ‘Haki’ ni Kala
Jeremiah, Quck Rocker, G-Nako, Nikki wa Pili, Mwana Fa, Danny Msimamo,
Profesa Jay, Gosby, Joh Makini, Fid Q na Kala Pina.
‘Haki’ imetayarishwa ndani ya Bongo Records na mtayarishaji mkongwe P-Funk Majani.
Kwa mujibu wa John Kitime, mwanamuziki mkongwe wa Tanzania, wasanii
wamepanga kuwa na mkutano na waandishi wa habari (press conference) na
kuzindua wimbo huo.
Social Plugin