Moja kati ya surprises zilizokuwepo wiki iliyopita ni pamoja na habari ya Lady Jay Dee aka Anaconda kujifua kikomando kuumudu mchezo wa Karate, habari iliyoambatana na picha zikimuonesha akifundishwa mchezo huo tena akiwa ndani ya mavazi rasmi.
Itakuwaje
Jide akishakuwa fiti kwenye mitindo hatari ya karate kama Shotokan,
Wado-ryu, Shito-ry na Goju-ryu? Na je, anataka kumkabili nani hasa? Haya
ni kati ya maswali ambayo wengi tulijiuliza.
“Kwa
sababu ninao muda wa ziada, halafu kukaa tu idol bila kufanya kitu saa
zingine inaweza kupelekea mawazo yako kufikiria vitu vibaya. Kwa hiyo
nikaona sio vibaya nikifanya mazoezi.” Alisema Lady Jay Dee aka
Anaconda.
Alipoulizwa kama kuna mtu anataka kupigana naye alisema hakuna mtu ila anajiweka fiti tayari kwa lolote.
“Hapana
ni kutaka kujiweka fiti unajua kufanya mazoezi sio kwa ajili ya kutaka
kupigana na mtu, ni wewe mwenyewe tu uwe vizuri ili jambo likitokea
ujue jinsi ya kuji-protect.” Ameeleza.
Mkali huyo wa Joto Hasira amedai kuwa ana mwalimu mzuri na kwamba yeye pia ni mwanafunzi mwenye bidii.
credit: babamzazi
Social Plugin