Mtu aliyekuwa akituhumiwa kwa tuhuma za mauaji Mkoa wa Mara, Charles Kichune (38), ambaye alikufa mikononi mwa polisi amezikwa na halmashauri baada ya kukosa ndugu tangu mwili wake ulipohifadhiwa katika chumba cha maiti.
Mwili wa marehemu Kichune Mkazi wa Kijiji cha Kenyamanyori Wilaya ya Tarime aliyedaiwa kuua zaidi ya watu 11 kwa risasi ulihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika mji huo kwa zaidi ya siku tano tangu aliporipotiwa kufariki dunia.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime, Robert Onesmo alisema kuwa hospitali hiyo ilifikia uamuzi huo baada ya kuona hakuna ndugu ambaye amekuja kujitambulisha na kuuchukua mwili wa marehemu tangu kutokea kwa kifo hicho.
Muuaji huyo aliyekamatiwa mkoani Tanga akiwa anatoroka kwa mujibu wa taarifa kutoka polisi, alikufa kutokana na ugonjwa wa pumu.
Mtunza Mochwari, Samuel Marindi alisema kuwa mwili wa marehemu huyo ulizikwa jana mchana kwenye makaburi ya Ronsont, Tarime.
Hata hivyo, Marindi alisema mwili huo ulishindikana kuzikwa katika kijiji chake kutokana na wenye magari kugoma kumbeba na wananchi kukataa kumpitisha mitaa ya Mji wa Tarime.
>>Mwananchi
>>Mwananchi
Social Plugin