Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Majanga!! MWANAMME ALIYEKUTWA UCHI AKIFUKUA KABURI LA MWANAMKE AFIKISHWA MAHAKAMANI

Mkazi wa kijiji cha Ikola  Wilaya ya Mpanda Mkoa  wa Katavi  Richard  Clavery  34 amefikishwa  Mahakamani  katika mahakama ya Wilaya ya Mpanda kujituhuma za kufanya vitendo vya ushirikina  wa kufukua kaburi la mwanamke alikufa
Mtuhumiwa  alifikishwa kizimbani hapo Februari   25 mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa   na kusomewa mashitaka na mwendesha mashitaka  Godfrey  Luzabila
Mwendesha mashitaka alidai  Mahakamani hapo kuwa  mtuhumiwa  alitenda kosa hilo hapo Februali   18 mwaka huu majira ya saa nne usiku nyumbani kwa  Lenada  Sakafu
Mwendesha mashitaka   Luzabila  aliiambia mahakama kuwa siku  hiyo ya tukio  mtuhumiwa alifika nyumbani kwa Lenada  Sakafu  na kufukua  maiti ya mdogo wake na Lenada  aitwaye Tabu Omera  ambae alikuwa amefarii  siku tatu kabla ya tukio  hili
Aliendelea kuieleza Mahakama   siku hiyo  Lenanda  alikuwa nyumbani  kwake pamoja na   majirani na ndugu  zake wakiendelea kuomboleza msiba  ghafla alitokea  mtoto wake aitwaye  Brandina  na kuwaeleza  kuwa ameona mtu nje akifukua kaburi la marehemu   ambae alikuwa amezikiwa  kwenye eneo la nyumba yao
Alieleza ndipo watu hao walipoamua kutoka nje   na kumkuta  mtuhumiwa  Richard  Clavery   akifukua kaburi  hilo huku akiwa  amevua nguo zake zote  ambazo alikuwa amezitundika kwenye msalaba  wa kaburi  hilo  na walipomsemesha mtuhumiwa  alijifanya kupandisha majini
Mtuhumiwa  baada ya kusomewamashitaka  alikana   na Hakimu Mkazi Mfawidhi  Chiganga Ntengwa aliharisha kesi hiyo hadi hapo machi 6 na mtehumiwa alipelekwa lumande  baada ya kushindwa kutimiz mashariti ya mdhamana ambapo alitakiwa adhaminiwe na mtu mmoja kwa  dhamana ya shilingi milioni  moja.
 N a Walter  Mguluchuma-Katavi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com