NB-picha haiendani na habari hapa chini |
Ikiwa ni takribani wiki moja imepita baada ya kaya 5 katika kijiji cha Kakeneno
kata ya Buziku wilayani Chato kuchomwa moto
na wananchi kwa kisingizio cha kwamba wamiliki wake ni wachawi katika hali ya
kushangaza vitendo hivyo vimezidi kujitokeza safari hii ni katika kijiji cha kilombero 2 ambapo kaya 7 zimeteketezwa
kwa moto Februari 15 mwaka huu.
Kitendo hicho kinachohusishwa na imani za
kishirikina kimezua tafrani katika kijiji hicho na
kimesababisha baadhi ya wakazi wa eneo hilo kutoroka na kukimbia
kusikojulikana.
Chanzo cha tukio la kuchomwa moto nyumba
hizo kumetokana na tukio la mwanamke mmoja aitwaye Felister Mathias kuuawa kwa
kukatwa katwa mapanga mwanzoni mwa mwezi huu.
Akizungumzia kuhusu chanzo cha tukio hilo
afisa mtendaji wa kijiji cha kilombero 2 Matiba alisema kuwa mama huyo inadaiwa
kuwa mifugo yake iliingia kwenye shamba la jirani yake na baada ya hapo
wakapelekana kwenye vyombo vya sheria na mama huyo akakiri kulipa kisheria.
“Cha kushangaza baada ya muda mlipwaji(jirani)
alikataa kumlipa kisheria na alitaka amlipe kimya kimya lakini mama huyo
alikataa na kabla ya siku waliyoahidiana kulipa mama huyo alikatwakatwa mapanga
huku wakidhani kuwa ni mshirikina”,alieeleza afisa mtendaji.
Ameongeza kuwa baada ya tukio hilo baadhi
ya watu waliokamatwa na jeshi la polisi wakihusishwa na tukio hilo walipelekwa
kituoni .
“Kufuatia kukamatwa kwa wanachi,baadahi ya
wananchi waliosalia walihisi kuna watu
wamesababisha wenzao kukamatwa wakaanza kualikana na kuanza kuchoma nyumba
baadhi ya kaya walizokuwa wanadhani ni chanzo cha mgogoro huo tarehe 15 mwezi
huu”,aliongeza.
Kwa upande wa diwani wa kata ya Rwamgasa
kilipo kijiji hicho Christopher Kadeo alipoulizwa juu ya tukio hilo amesema
kuwa hajui kama kuna kitu cha namna hiyo.
Kwa upande wa katibu wa shirika lisilo la
kiserikali linalotoa msaada wa kisheria na
haki za binadamu wilayani Geita Elineema Charles alisema ni vyema vitendo hivi
vikakemewa na jamii pamoja na serikali kwani vimekuwa vikijirudia mara kwa
mara.
Baadhi ya kaya zilizochomwa ni pamoja na familia
ya Hamis Kisumo,kisumo sama,Elias Kisumo,Shija sahani,Luka Ngodagula,Orogwe Kisumo
ambaye ni mtemi wa sungusungu, na India Sahani, Will itenga huku baadhi yao
wakiwa wamekimbia makazi yao.
Kufuatia kuchomwa kwa kaya hizo 7 mkuu wa
wilaya ya Geita Manzie Omari Mangochie mkoani Geita ametoa siku kumi kwa
viongozi wa kijiji cha kilombero 2 kuhakikisha wanawatafuta na kuwakamata
watuhumiwa kwa namna yoyote kwani hapo kijijini wanajuana tabia zao.
Mkuu huyo ametoa agizo hilo mapema juzi
mara baada ya kutembelea kaya saba zilizochomwa moto na wananchi wenye hasira
kali kutokana na chanzo chake kikiwa ni imani za kishirikina.
Imeelezwa kuwa kijiji hicho matukio ya
namna hiyo yanatokea sana ambapo hilo ni tukio la 5 katika muda wa miezi 12.
Na Valence Robert-Geita
Na Valence Robert-Geita
Social Plugin