Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangalla |
Wanawake wawili wakazi wa kijiji cha Ngokolo kata ya Bukomela wilaya
ya Kahama mkoani Shinyanga wameuawa kikatili kwa kukatwa katwa mapanga sehemu za kichwani na kisogoni na watu wasiojulikana
wakati wakipika chakula cha usiku nyumbani kwao.
Tukio hilo limetokea juzi saa moja na nusu usiku ambapo wanwake hao (mama
na mwanaye) walivamiwa na watu hao kisha kufanya unyama huo na kutokomea kusikojulikana.
Kamanda wa polisi mkoa wa
Shinyanga SACP Evarist Mangala amewataja
wanawake waliouawa kuwa ni Helena Charles(30) na mama yake aitwaye Mlu Nambo(50) wote
wakazi wa kijiji cha Ngokolo ambao walifariki dunia papo hapo kufuatia kuvuja
damu nyingi.
Aidha amesema chanzo cha mauaji
hayo bado kinachunguzwa na tayari mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi na
wengine waliohusika na mauaji hayo wanaendelea kusakwa.
Social Plugin