Mbeya City |
Simba ya Jijini Dar es salaam |
Mapato kwa mechi ya
ligi ya Vodacom kati ya timu za Mbeya City ya Jijini Mbeya na Simba ya Jijini
Dar es salaam yamevunja rekodi ya michezo yote iliyowahi kuchezwa nje ya Jiji
la Dar es salaam kwa kuingiza kiasi cha sh. milioni 105.
Mechi iliyowahi
kuingiza kiasi kikubwa cha mapato katika uwanja huo ni ile iliyochezwa kati ya
Timu ya Mbeya City na Yanga ya Dar es salaam katika uwanja huo mwaka jana na
kuingiza kiasi cha sh. milioni 100.
Katika mapato hayo
kila timu ilipata kitita cha sh. milioni 25.3 ambapo sh.milioni 12.8 zilibaki
kwa ajili ya uwanja,sh.milioni 7.7 kwa ajili ya maandalizi na sh. milioni 7.7
kwa ajili ya kamati ya ligi ilhali sh. milioni 3.8 zilikuwa ni kwa ajili ya chama
cha mpira wa miguu TFF.
Na Steve Kanyefu
|
Social Plugin