Mmiliki wa Microsoft Bill Gates amejiondoa kama mwenyekiti wa kampuni yake ya Microsoft na kushika wadhifa mpya kama mshauri wa teknolojia.
Satya Nadella ametajwa kuwa mwenyekiti mtendaji mkuu wa kampuni hiyo.
Tangazo la CEO mpya limekuja baada ya aliyekuwepo Steve Ballmer kutangaza mwaka jana nia yake ya kustafu.
Nadella anakuwa mwenyekiti mtendaji wa tatu katika historia ya miaka 39 ya Microsoft, baada ya mwanzilishi mwenza Bill Gates na Steve Ballmer.
Microsoft imesema John Thompson atachukua nafasi ya uenyekiti iliyoachwa na Bill Gates.
Social Plugin