Kamanda wa polisi mkoa wa Geita-Leonard Paul |
Jeshi la polisi mkoani Geita limewaomba
wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo katika misako inayoendelea
kufanywa na jeshi la polisi ambapo kati ya tarehe 22 hadi 28 mwezi januari
wamefanikiwa kukamata wahalifu 10.
Wito huo umetolewa na kamanda wa polisi
mkoa wa Geita Leonard Paul wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa
habari kuhusu kukamatwa kwa wahalifu mkoani Geita ambapo wananchi kwa
kushirikiana na jeshi hilo wamefanikiwa kuwatia mbaroni watu kumi katika
kipindi hicho cha Januari 22 hadi 28 mwaka huu.
Kamanda Paul amewataja watuhumiwa wa uhalifu
wa aina mbalimbali waliokamatwa kuwa ni
Goodluck Faustine(18) Venance Daniel(18) Fabiani Raphaeli(18) Hamis Idd(18)
George Manase(19) Abeid Prosper(19)Kashindye Juma(20) Faida Charles(20) Mhoja Kadogo(19)
na Baasi Ally(18).
Kamanda amevitaja vitu ambavyo watuhumiwa
hao wamekamatwa navyo kuwa ni pamoja na Tv flat screen 4, tv
za kawaida 3 ,deck za dvd 4 sub-woofer 2 simu za mkononi 2, mashine ya kunyolea
1 ,vifaa vya kuvunjia nyumba ambavyo ni sululu 1,nondo1 mkasi mkubwa 1, spana5
plaiz 1 na tayari baadhi ya wananchi wameanza kuvitambua vitu vyao vilivyoibiwa.
Katika hatua nyingine baadhi ya wananchi katika
mkoa wa Geita wamesema wamekuwa wakishangazwa kuona watuhumiwa wengi kuwa na
umri unaofanana na hiyo yote inatokana na lindi la vijana ambao hawana kazi
kujiingiza katika uharifu ili waweze kujipatia vipato vya kujikimu.
Kwa upande wake ambaye ni katibu wa
shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za binadamu wilayani Geita Bwana
Elineema Charles amesema kutokana na mji wa Geita sasa hivi unavyokuwa kwa kasi
ni vyema jeshi la polisi likashirikiana
na raia ili kufichua vitendo vya uharifu ambavyo vinaweza kuhatarisha sio mali
tu za wananchi lakini hata maisha.
Hata hivyo bw charles ameongeza kuwa
ushiriki wa kamanda wa polisi mkoani Geita ni vyema ukaigwa na askari wote wa
mkoa huu hata nchi kwa ujumla kwani kila mara amekuwa mwepesi wa kufika kwenye
matukio mbalimbali yanayojiri katika mkoa huo kwa kujionea mwenyewe na si
kuambiwa kama walivyo wengine.
Na Valence Robert-Geita
Social Plugin